• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mwanamke kuchezesha kwa mara ya kwanza ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1)

    (GMT+08:00) 2019-04-25 09:54:42
    Kwa mara ya kwanza wikiendi hii inayokuja, ligi kuu ya soka ya wanaume nchini Ufaransa, itachezeshwa na refa mwanamke, Stephanie Frappart atakapopuliza kipenga katika mechi baina ya Amiens na Strasbourg.

    Shirikisho la soka la Ufaransa (FFF) limetangaza kuwa uteuzi wa refa wa mechi hiyo ya Jumapili, unatokana na ombi kutoka shirikisho la soka duniani (FIFA) kusaidia waamuzi watakaochezesha fainali za kombe la dunia kujiandaa katika mazingira bora kwa ajili ya michuano hiyo.

    Mwamuzi wa Ujerumani, Bibiana Steinhaus alikuwa refa wa kwanza mwanamke katika ligi kubwa barani Ulaya baada ya kuchezesha mechi ya ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga) kati ya Hertha Berlin na Werder Bremen mwezi Septemba mwaka 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako