• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya KCB kuinunua benki ya National,huenda wengi wakapoteza ajira

    (GMT+08:00) 2019-04-25 20:44:08
    Inahofiwa kuwa watu wengi zaidi katika sekta ya benki huenda wakapoteza ajira kutokana na ongezeko la Benki zinazoungana.

    Haya yamejiri baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Joshua Oigara kutangaza nia ya kununua Benki ya National (NBK).

    Alisema pendekezo hilo la kununua NBK litaunganisha zaidi sekta hiyo na litaimarisha mashirika na kuwezesha KCB kuwa na nafasi kubwa ya kukuza uwezo wa idadi ya watu wanaotumia huduma za benki.

    Takwimu kutoka Benki Kuu ya Kenya zinaonyesha kuwa zaidi ya kupoteza kazi kutokana na benki kutofanya vyema, benki zilizosalia zinaendelea kupunguza nafasi za kazi kwa lengo la kukabiliana na gharama kubwa ya operesheni.

    Hii ni kutokana na kudhibitiwa kwa viwango vya riba na matumizi ya mfumo wa kidijitali.

    Katika muda wa miaka mitatu kufikia Desemba 2017, benki zimefuta kazi wafanyikazi 6,020 na wafanyikazi zaidi huenda wamepoteza kazi mwaka wa 2018 na 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako