Akizungumza jana, Afisa Biashara, Thomas Mcharo, ambaye ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya mtangamano wa biashara Wizara ya Viwanda na Biashara, alieleza kuwa lengo la kuanzishwa biashara ya pamoja kwa jumuiya hizo ni kukuza uchumi.
Alisema biashara hiyo imegawanyika katika hatua tatu, ambayo ni asilimia 90 ya bidhaa zinazopatikana kwa wanachama wa jumuiya hiyo kutotozwa ushuru katika vituo vya forodha, asilimia tatu watalipia kwa awamu na asilimia saba hazitofunguliwa.
Mcharo alisema biashara huru itaisaidia Tanzania kutokana na mkakati wake wa kuingia katika uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda, kwa kuwa viwanda vitazalisha na kutakuwa na masoko ya kutosha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |