• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi Kuu Tanzania Bara –Simba yaendeleza kula viporo, yaitandika KMC, yaishusha Azam FC nafasi ya pili.

    (GMT+08:00) 2019-04-26 08:28:04
    Emmanuel Okwi anazidi kudhihirisha anajua anachokifanya akiwa uwanjani baada ya jana kuifungia timu yake bao moja kati ya mawili ambayo Simba ya Dar es Salaam iliifunga KMC katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

    Okwi alifunga bao dakika ya 23 akimalizia pasi ya James Kotei. KMC ilipata bao la kusawazisha kupitia kwa Hassan Kabunda akitumia makossa ya beki wa Simba Zana Coulibary. Simba ilipata Penalti dakika ya 75 baada ya mchezaji wa KMC kuunawa mpira ndani ya 18, lakini mkwaju huo wa penalti ulidakwa na golikipa wa KMC Jonathan Nahimana.

    Dakika saba mbele Mzamiru Yassin alitengeneza penalti nyingine na nahodha John Bocco alipachika wavuni na kufanya Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 na kupelekea kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, ikiishusha Azam FC

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako