• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Wachezaji Yanga wagomea mazoezi, Zahera avunja ukimya

    (GMT+08:00) 2019-04-26 08:28:58
    Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema uamuzi wa wachezaji wa klabu hiyo kugomea mazoezi sababu ya kutolipwa mishahara yao kwa zaidi ya miezi minne kimemkera kwakuwa wachezaji hao hawakumshirikisha.

    Wachezaji wa Yanga jana walifika mazoezini asubuhi lakini hawakufanya mazoezi wakishinikiza kulipwa mishahara yao. Zahera amefunguka kuchukizwa na kitendo hicho, aidha amepiga mkwara kuwa, wachezaji ambao leo hawataenda mazoezini atawafukuza moja kwa moja kwasababu hawana nia ya kuichezea klabu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako