• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Boda boda kuanzisha benki yao.

    (GMT+08:00) 2019-04-26 20:31:50
    LICHA ya kusababisha ajali na madhara makubwa kwa watumiaji wake, na waendeshaji biashara ya pikipiki maarufu kama bodaboda imetajwa na taasisi nyingi kuwa ni biashara inayolipa kwa wawekezaji na inatoa ajira kubwa kwa idadi kubwa ya vijana nchini Tanzania; na sasa inataka kujiongeza kwa kuwa na benki yao yenyewe. Nchi nzima Dar es Salaam ndiko kwenye boda boda nyingi ingawa idadi yao haijulikani kwa sasa na juhudi inafanywa kupata takwimu sahihi lakini inakisiwa kuwa zaidi ya 50,000.

    Mwenyekiti wa chama cha madereva na wamiliki wa pikipiki Mkoa wa Dar es salaam (CMPD) Michael Masawe amesema chama hicho kimeanza mchakato wa kufungua benki kwaajili ya madereva pikipiki maarufu kama bodaboda. kila dereva wa pikipiki atatoa Sh.500 kila siku kwaajili ya kuhifadhiwa kwenye benki hii ili itasaidia baadaye kupata mkopo nafuu na kuweka akiba kwaajili ya kesho yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako