• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Kenya haikamatiki katika ramani za mbio, Ni Kipchoge tena na Kosgei

    (GMT+08:00) 2019-04-29 08:05:30

    Bingwa wa mbio za Olimpiki toka Kenya Eliud Kipchoge ameudhihirishia ulimwengu kuwa hakamatiki kirahisi baada ya kuweka rekodi nyingine tena mwishoni mwa wikiendi katika mashindano ya riadha ya London yaliyofanyika nchini Uingereza.

    Kipchoge aliwaacha Muethiopia Mosinet Geremew na Mule Wasihun alipomaliza na kuwa mshindi kwa kutumia masaa 02:02:37. Kwa upande wa wanawake, mwanadada Brigid Kosgei mwenye umri wa miaka 25 amefanya maajabu baada ya kuwashinda wakubwa wake katika mashindano hayo baada ya kutumia 02:18:19 na kumshinda mkenya mwenzake Vivian Cheruiyot aliyetumia 02:20:51 huku muethiopia Roza Dereje amekamata nafasi ya tatu kwa kutumia 02:20:51

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako