• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa China na Austria wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2019-04-29 09:05:18

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana hapa Beijing amefanya mazungumzo na mwenzake wa Austria Bw. Sebastian Kurz.

    Bw. Li amesema, Austria ni mwenzi muhimu wa ushirkiano wa China barani Ulaya, na nchi hizo mbili zina mustakabali mzuri wa ushirkiano kwenye utengenezaji wa kisasa, kilimo na utalii.

    Kwa upande wake Bw. Kurz amepongeza mafanikio ya mkutano wa pili wa kilele wa Baraza la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Amesema, Austria inaipongeza China kwa mafanikio makubwa iliyopata, na inapenda kuimarisha ushirikiano na nchi hiyo kwenye sekta za uchumi na biashara, kilimo, utalii na michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, ili kuhimiza maendeleo mapya ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako