• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ahudhuria na kuhutubia ufunguzi wa Maonyesho ya kimataifa ya kilimo na maua ya Beijing

    (GMT+08:00) 2019-04-29 09:43:12

    Rais Xi Jinping wa China jana alihudhuria na kuhutubia ufunguzi wa Maonyesho ya kimataifa ya kilimo cha maua ya mwaka 2019 ya Beijing, na kutoa hotuba muhimu yenye kaulimbiu ya "Kutafuta Maisha ya Kijani na Kujenga kwa pamoja Maskani Mazuri ya Binadamu".

    Katika hotuba yake, rais Xi amesema sayari ya dunia ni maskani pekee kwa binadamu, na ni lazima kulinda mazingira ya kiikolojia, kuweka msingi wa ustaarabu wa kiikolojia na kuhimiza kwa pamoja maendeleo yasiyosababisha uchafuzi. Amesema inapaswa kujenga uhusiano wa masikilizano kati ya binadamu na maumbile, kutafuta ustawi na maendeleo yasiyoleta uchafuzi, kupenda mazingira ya asili, kutafuta utatuzi kwa njia mwafaka, na kushirikiana katika kukabiliana na changamoto inayowakabili binadamu.

    Amesisitiza kuwa maendeleo ya pamoja ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja", yanatakiwa kujengwa kwa njia ya wazi ya maendeleo, na kwamba China inapenda kushirikiana na nchi zote duniani katika kujenga kwa pamoja maskani mazuri ya binadamu duniani na jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako