• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namna ya kuitikia wito wa kujenga "Maskani Mazuri ya Binadamu Duniani"

    (GMT+08:00) 2019-04-29 14:40:20

    Ijumaa iliyopita, maonesho ya kimataifa ya kilimo cha maua ya mwaka 2019 yalifunguliwa hapa Beijing, yakiwa na kaulimbiu "Maisha yasiyo na uchafuzi, Maskani Mazuri ya Binadamu". Nchi na mashirika ya kimataifa 110 yanayoshiriki kwenye maonesho hayo yameonesha mimea ya aina mpya zaidi ya 1,200.

    Akihutubia ufunguzi wa maonesho hayo, rais Xi Jinping wa China alitoa wito wa "kujenga kwa pamoja maskani mazuri ya binadamu duniani, kujenga kwa pamoja jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja".

    Mwaka 2012, Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China uliuweka ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia kwenye mpango wa jumla wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na dhana ya rais Xi Jinping ya "Maji safi na milima ya kijani ni hazina kubwa" imepata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wananchi wa China. Mwaka 2018, ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia ulijumuishwa kwenye mswada wa marekebisho ya Katiba ya China.

    Katika miaka ya hivi karibuni, ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia nchini China umeingia kwenye njia ya kasi, ambapo uchafuzi umepungua na mazingira yameboreka. Takwimu za satelaiti zilizotolewa na Shirika la anga za juu la Marekani NASA, zimeonesha kuwa, ikilinganishwa na miaka 20 iliyopita, eneo la misitu duniani limeendelea kuongezeka, na moja ya sababu kuu ni shughuli za upandaji miti nchini China.

    Ndio ni kama alivyosema rais Xi Jinping kwamba "Mbele ya changamoto za kiikolojia, binadamu wote ni jumuiya yenye mustakbali wa pamoja, na hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kujitenga na mustakbali wa pamoja." Mfano wa wazi ni mabadiliko ya hali ya hewa, ambayo yametoa changamoto kubwa kwa nchi nyingi, haswa baadhi ya nchi za visiwa. Ni dhahiri kuwa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ni jukumu na wajibu wa nchi zote duniani.

    Viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano wa Ukanda mmoja Njia moja uliomalizika Jumamosi hapa Beijing, wamefikia maafikiano kuwa "Ukanda mmoja Njia moja" si kama tu inapaswa kujengwa kuwa njia ya wazi ya maendeleo, na bali pia inatakiwa kuwa njia ya kutafuta maendeleo yasiyochafua mazingira, kwa sababu maendeleo yasiyo na uchafuzi si kama tu yanahusiana na maslahi ya watu wa sasa, na bali pia yanahusiana na mustakbali wa binadamu wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako