• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chombo cha safari ya anga ya juu cha China Chang'e -4 chaanza kazi katika siku ya tano

    (GMT+08:00) 2019-04-29 19:03:08

    Chombo cha anga ya juu cha China Chang'e -4 kimeanza kazi kwenye siku ya tano ya mwezi, kwenye upande wa mbali wa mwezi, baada ya kulala wakati wa usiku wenye baridi kali.

    Kituo cha utafiti wa mwezi na mpango wa anga wa juu wa China kimesema, chombo cha kutua kwenye mwezi kimeamka leo asubuhi, na chombo kinachotembea kwenye mwezi kiliamka jana mchana, na vyote vinaendelea kufanya kazi vizuri.

    Mpaka sasa kifaa hicho kimetembea mita 178.9 kwenye mwezi, na kufanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

    Siku moja ya mwezi ni sawa na siku 14 duniani, na usiku mwa mwezi pia una muda kama huo. Chombo cha Chang'e kilizimwa baada ya kukosa mwanga wa jua kutokana na giza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako