• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda- EgyptAir yazindua safari mbili kwa wiki kwenda Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-04-29 19:46:22

    Shirika la ndege la Misri EgyptAir limezindua safari mbili kwa wiki kwenda mjini Kigali Rwanda katika juhudi za kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili.

    Safari ya kwanza ya shirika hilo kwa kutumia ndege aina ya Boeing 737-800 imefanyika Jumapili.

    Waziri wa uchukuzi wa Rwanda Jean de Dieu Uwihanganye, amesema huduma za shirika hilo ni dhihirisho kuwa Rwanda imekuwa kituo muhimu cha kikanda katika usaifiri wa anga.

    Kulingana na mkurungezi mkuu wa EgyptAir Ahmed Adel, ndege inayohudumu kwenda Kigali imepambwa na picha za wachezaji wa timu ya taifa kama ishara ya kushambikia mashindano ya kombe la Afrika yatakayofanyika mwezi Juni nchini Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako