• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali kuhamasisha wakaazi kutenga maeneo ya miundombinu ya gesi

    (GMT+08:00) 2019-04-29 19:46:50

    Waziri wa Nishati wa Tanzania Dk. Medard Kalemani, ameliagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kuwatumia viongozi wa serikali za mitaa ili wakawahamasishe wananchi waweze kutoa maeneo yao kwa ajili ya upitishaji wa miundombinu ya gesi asilia.

    Pia, amelitaka shirika hilo kuhakikisha katika kipindi cha miaka miwili robo ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wawe wameshaunganishwa na mfumo wa utumiaji wa gesi asilia.

    Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya ukaguzi wa usambazaji wa miundombinu ya gesi asilia katika maeneo ya Mikocheni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), pamoja na Mlalakua.

    Alisema serikali imeshatenga Sh. trilioni moja kwa ajili ya kusambaza gesi asilia kwa wananchi, na kwamba mikakati iliyopo ni kusambaza gesi katika viwanda vyote vya Jiji la Dar es Salaam, na kwa sasa imeanza na kiwanda cha Coca Cola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako