Chama cha wenye benki nchini Uganda kimesema kuwa sekta hiyo hupoteza shilingi bilioni 400 kila mwaka kutokana na kesi mahakamani .
Mwenyekiti wa chama hicho Patrick Mweherie, amesema asilimia 50 hado 70 ya mitaji ya benki huzuiliwa na mahakama kwenye kesi ambazo huchukua muda mrefu.
Alisema kwenye hali hiyo mitaji husalia kwenye benki bila kuendeleza biashara yoyyote hadi kesi inapoamuliwa.
Bwana Mweherie alisema kuwa sekta ya benki nchini humo imeathrika na kuongezeka kwa gharama za kufanya biashara ambazo zinafikia asilimi 78 ikilinganishwa na watani wa kote duniani wa asilimia 50.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |