• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wadau wa kusaga unga kukutana na serikali

    (GMT+08:00) 2019-04-29 19:53:49

    Wizara ya kilimo nchini Kenya itandaa mkutano wa pili na wasagaji kesho ili kukubaliana kuhusu taratibu za kutolewa kwa mahindi kwa bei nafuu kutoka kwa ghala la kitaifa.

    Wizara hiyo imesema hatua hiyo itasaidia kupunguzwa kwa bei ya unga wa mahindi.

    Katibu wa kudumu kwenye wizara ya kilimo Profesa Hamadi Boga, amesema kuwa wenyekiti wa kampuni za kusaga unga wamealikwa kwenye mkutano huo utakaoongozwa na waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri.

    Kwa sasa bei ya mahindi imefikia shilingi 3,400 kwa gunia la kilo 90 ikilinganishwa na 2,300 za mwezi Machi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako