• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yafuatilia hotuba aliyoitoa rais Xi katika ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo cha Maua ya Beijing

    (GMT+08:00) 2019-04-30 09:53:49

    Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo cha Maua ya Mwaka 2019 yamefunguliwa tarehe 28 mjini Beijing, China. Akihutubia ufunguzi wa maonesho hayo Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kujenga ustaarabu wa kiikolojia na kutafuta maendeleo kwa njia isiyochafua mazingira.

    Mwenyekiti wa Chama cha kimataifa cha wazalishaji wa kilimo cha bustani Bw. Bernard Ostrom amesema, China inaongoza katika kutafuta maendeleo yasiyo na uchafuzi wa mazingira. Ameongeza kuwa Maonesho hayo yamewaleta watu pamoja na kufanya juhudi kwa ajili ya kazi za pamoja. Anaamini kuwa maonesho hayo yataifanya dunia kufuatilia namna China inavyoboresha mazingira ili kuwafanya wananchi waishi vizuri zaidi.

    Mtaalamu wa Kenya anayeshughulikia mambo ya China na Afrika Bw. Edhurley Cavens pia amesema, hotuba ya rais Xi imewafanya watu watambue dhamira ya China katika kutilia maanani ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako