• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • MASUMBWI: Mwakinyo ni habari nyingine, aongoza kwa ubora Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-30 10:07:42

    Nyota ya bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo inazidi kung'ara, Mwakinyo ameendelea kushikilia rekodi ya kuwa bondia namba moja Afrika akiwa na alama 152.1 akiwapiku mabondia wengine 123 kwenye uzani wake katika viwango vilivyotolewa na shirikisho la ngumi duniani.

    Bondia wa Afrika Kusini Emmany Kalombo anashika nafasi ya pili akiwa na alama 126.8 huku Charles Manyuci wa Zimbabwe anashikilia namba tatu ya ubora Afrika akiwa na alama 114.5

    Kwenye viwango vya dunia, Mwakinyo anakamata nafasi ya 24 akiwa ameporomoka nafasi nane tangu alipopanda na kuwa wa 16 mwaka jana alipomchapa Eggington.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako