• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Ethiopia na Kenya bado zatamba katika riadha, Mtanzania akamata nafasi ya tatu

    (GMT+08:00) 2019-04-30 10:08:13

    Mwanariadha wa Tanzania Failuna Abdi ameng'ara katika mbio za Haspa Hamburg zilizofanyika nchini Ujerumani huku akivunja rekodi ya muda wake wa awali.

    Failuna mwanariadha wa timu ya taifa ya riadha ya Tanzania ametwaa medali ya shaba kwenye mbio hizo za fedha akitumia saa 02:27:56

    Katika mbio hizo, Failuna aliachwa kwa dakika 3:14 na mwanariadha wa Ethiopia Dibabe Kaima. Dibabe ametumia saa 02:24:42 kumaliza mbio hizo na kutwaa medali ya dhahabu huku Magdalyne Masai toka Kenya akikamata nafasi ya pili kwa kutumia saa 02:26:04

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako