• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania kufuta mikopo

    (GMT+08:00) 2019-04-30 19:50:49

    Serikali ya Tanzania imesema inakusudia kuyafuta malimbikizo ya fedha za mikopo ya vijana na wanawake ya miaka ya nyuma iliyotakiwa kutolewa kabla ya mwaka 2016 lakini haikutolewa na halmashauri kwa walengwa.

    Hatua hiyo inatokana na maelekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kufuatia malimbikizo hayo kusababisha uwapo wa hoja za ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

    Kusudio hilo lilitangazwa bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Mwita Waitara. Madeni ya halmahauri hususani mikopo ya vijana na wanawake ya miaka ya nyuma kabla ya 2016 yamekuwa hayalipiki kutokana na halmashauri nyingi kutokuwa na mapato ya kutosha kuendesha halmashauri hizo hasa miradi ya maendeleo.

    Waitara alisema kwa sasa, kazi ya uhakiki wa takwimu kubaini kiasi ambacho kimelimbikizwa katika halmashauri zote nchini inaendelea na mara tu itakapokamilika taratibu za kufuta malimbikizo hayo zitafanyika.

    Alisema kwa sasa, Ofisi ya Rais, Tamisemi inazisimamia kwa karibu halmashauri ili kuhakikisha zinatoa fedha hizo kwa mujibu wa sheria ambayo inasimamia utoaji mikopo hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako