• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kukuza elimu ya ufundi stadi na kupanua usajili wa wanafunzi katika vyuo vya ufundi stadi

    (GMT+08:00) 2019-05-01 09:24:54

    China itatumia Yuan bilioni 100, sawa na dola za kimarekani bilioni 15 kutoka kwenye akiba ya Mfuko wa Bima ya Ukosefu wa Ajira kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi ili kuongeza uwezo wa wafanyakazi wa China katika kupata kazi au kuanzisha biashara. Uamuzi huu umefanywa kwenye mkutano wa utendaji wa Baraza la Serikali la China ulioendeshwa na waziri mkuu Li Keqiang. Utekelezaji wa mpango wa kupanua idadi ya wanafunzi wanaosajiliwa katika vyuo vya ufundi stadi kwa milioni moja mwaka huu, pia umeridhiwa kwenye mkutano huo ili kuandaa vipaji vya ufundi stadi wa aina mbalimbali na kuongeza nafasi za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako