• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asema maingiliano ya kitamaduni ni nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu

    (GMT+08:00) 2019-05-01 10:10:40

    Jarida la Chama cha Kikomunisti cha China Qiushi limechapisha makala ya rais Xi Jinping wa China yenye kichwa kisemacho "Maingiliano kati ya tamaduni ni nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu na amani ya dunia".

    Makala hiyo imesema ni lazima kuhimiza tamaduni tofauti ziheshimiane, kusikilizana, na kufanya maingiliano kati ya tamaduni yawe daraja la kuimarisha urafiki kati ya watu wa nchi mbalimbali, kuhimiza maendeleo ya jamii ya binadamu na kulinda amani ya dunia. Makala pia imesema kuhimiza kufunzana kitamaduni kunapaswa kushikilia msimamo na kanuni sahihi, yaani tamaduni zina aina mbalimbali, ni za usawa na shirikishi. Imeongeza kuwa China inafanya utamaduni wa kichina ushirikiane na tamaduni za nchi nyingine katika kutoa mwongozo sahihi na msukumo mkubwa wa kiroho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako