• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gor Mahia yajihimarisha katika usukani wa ligi

    (GMT+08:00) 2019-05-01 10:36:55
    Vigogo wa Kenya Gor Mahia wamezidi kujikita kwenye uongozi wa ligi kuu nchini humo baada ya kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Ulinzi Stars mchezo uliopigwa uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

    Mganda Erisa Ssekisambu aliifungia Gor Mahia bao la kwanza katika dakika ya kwanza ya mchezo huku Ulinzi wakisawazisha dakika ya 76 kupitia Enosh Ochieng. Dakika nne kabla ya mchezo kumalizika, Samuel Onyango alikamilisha idadi ya mabao kwa Gor.

    Gor Mahia wanaongoza ligi hiyo kwa kuwa na alama 58 nao Ulinzi inaalama 36 ikiwa katika nafasi ya saba. Kesho Gor Mahia watavaana na KCB mjini Kisumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako