• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Jamhuri ya Dominica zapongezana kuadhimisha mwaka mmoja wa kuanzisha uhusiano wa kibalozi kati yao

    (GMT+08:00) 2019-05-01 18:50:05

    Rais Xi Jinping wa China na rais Danilo Medina wa Jamhuri ya Dominica wametumiana ujumbe wa kupongeza maadhimisho ya mwaka mmoja tangu nchi zao kuanzisha uhusiano wa kibalozi.

    Kwenye ujumbe wake Rais Xi amesema, China ilianzisha rasmi uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya Dominica mwezi Mei mwaka jana, na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Na kutokana na juhudi za pamoja kati ya pande hizo mbili, ushirikiano na mawasiliano katika sekta mbalimbali kati ya China na Jamhuri ya Dominica yanasonga mbele kwa utulivu, na kupata mafanikio makubwa. Rais Xi amesema atashirikiana na rais Medina kuimarisha ushirikiano wa kiwenzi kati ya nchi hizo mbili, kuhimiza maendeleo kwa pamoja, na kunufaisha nchi hizo mbili na raia wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako