• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba iliyotolewa na rais Xi yawatia moyo vijana wa China wanaoishi katika nchi za nje

    (GMT+08:00) 2019-05-02 10:18:21

    Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 100 ya vuguvugu la Mei 4. Vijana wanaosoma au kufanya kazi katika nchi za nje wamesisimuka baada ya kusikiliza hotuba hiyo, huku wakisema watabeba majukumu ya zama mpya na kutoa mchango katika ustawishaji wa taifa la China.

    Mwanafunzi wa China anayesoma shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Moscow nchini Russia Bw. Wang Yuehan amesema, hotuba ya rais Xi imewahamasisha wao kama vijana wa zama mpya kuweka lengo lenye mustakabali mkubwa, kubeba majukumu ya zama. Amesema wanatakiwa kuutilia maanani wito wake na kutoa mchango katika mchakato wa ujenzi wa nchi yenye nguvu ya kisasa ya Ujamaa na kutimiza ustawishaji wa taifa la China.

    Mwanafunzi anayesoma shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Long Island cha Marekani Bibi Sun Liyuan amesema, nchi ya unayozaliwa ni nguzo na tegemeo kwa wanafunzi wanaosoma katika nchi za nje. Uzalendo ni kiini cha moyo wa vuguvugu la Mei 4, ambao pia ni kiini cha moyo wa taifa. Wakiwa vijana wa China wa zama mpya, wanatakiwa kuleta miujiza mingi zaidi mapya kupitia juhudi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako