• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakulima waboreshewa kupata mikopo

    (GMT+08:00) 2019-05-02 18:47:51

    Wakulima nchini watapata fursa ya kukopa kutoka katika mabenki na taasisi za kifedha, baada ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB)kuingia katika makubaliano na Mfuko kichocheo wa SAGCOT CTF.

    Lengo kuu la makubaliano hayo ni kushirikiana katika kuboresha mazingira ya upatikanaji wa mikopo yenye tija kwa wakulima ili kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini.

    Akizungumza baada ya kusaini randama ya makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Sera wa TADB, Dk. Nyankomo Marwa, alisema makubaliano hayo ni hatua muhimu katika kuleta mageuzi na kuongeza tija katika sekta ya kilimo ambacho ni nguzo inayotegemewa kuchangiza maendeleo ya viwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako