• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA yaombwa kuanzisha dawati la kushughulikia changamoto

    (GMT+08:00) 2019-05-02 20:02:44

    Umoja wa Mawakala wa Forodha (TAFFA), Kanda ya Kaskazini, umeishauri Mamlaka ya Mapato (TRA), kuanzisha dawati maalumu la kushughulikia changamoto zinazowapata zikiwamo za mifumo ya mawasiliano ili kuwapunguzia gharama za kwenda mara kwa mara jijini Dar es Salaam.

    Katibu wa umoja huo Kanda ya Kaskazini, David Koyya, akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka alisema, kumekuwa na mkanganyiko wa namna ya kuwasiliana na taasisi za serikali, wanapokuwa katika majukumu ya kuwahudumia wateja wao ambao wanapenda mizigo yao ifike kwa wakati.

    Katibu Msaidizi wa Taffa, Michael Kwai, aliwataka watoa huduma za forodha katika mikoa ya kanda ya kaskazini, kujiunga na umoja huo ili uwe na nguvu katika kuwasiliana na serikali, ili kazi yao ifanyike kwa njia ya kitaalamu na kujenga imani kwa wateja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako