• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya ufaransa yapanga kuwekeza kwenye sekta ya kuhifadhi maziwa Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-05-02 20:03:39

    Kampuni moja ya ufaransa inapanga kuanzisha mradi wa kuhifadhi maziwa kwa kutumia kawi ya miale ya jua nchini Rwanda ili kupunguza gharama za umeme.

    Kampuni hiyo kwa jina Serap, imesema teknolojia hiyo itasaidia wakulima kuhifadhi maziwa yao na kufika sokoni kabla hayajaaribika.

    Ujumbe wa wajasiriamali wa sekta ya maziwa kutoka Ufaransa umefanya ziara nchini Rwanda ili kutathmini mazingira ya kibiashara kabla ya kuanzisha miradi hiyo.

    Mkuu wa mauzo wa kampuni ya Serap kwenye kanda ya afrika mashariki bwana Ali Haidar, amesema kila siku maelfu ya lita za maziwa kutoka kwa wakulima hukataliwa viwandani kutokana na ubora wa chini unaochangiwa na ukosefu wa njia bora za kuhifadhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako