• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Kampuni za Afrika Mashariki kuwekeza kusindika chai

    (GMT+08:00) 2019-05-02 20:04:47

    Kampuni tatu kubwa za chai kutoka nchi za Afrika Mashariki, zimejitokeza kuwekeza kwenye viwanda vya kusindika chai katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

    Kampuni hizo ni Dl group ya Kenya, Rwandan Mountain tea Ltd ya Rwanda, na E- vision Consulting ya Tanzania Ltd ambayo yamekuja Iringa baada ya mkoa kuwaita wawekezaji wa chai wilayani humo ili kuwanusuru wakulima wa chai wa wilaya hiyo.

    Ni mkutano ambao uliwakutanisha wawekezaji hao na uongozi wa mkoa wa Iringa ikiwa ni moja ya juhudi za serikali za kufufua kiwanda cha chai kilichopo wilayani humo kilichosimamisha uzalishaji kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita na kuwasababishia wakulima hasara kubwa.

    Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa, Hapiness Seneda, aliwashukuru wawekezaji waliojitokeza, akisema hatua hiyo inaashiria nia ya dhati ya kuwasaidia wakulima wa chai wa wilaya hiyo.

    Seneda alisema baada ya majadiliano ya muda mrefu walikubaliana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwamba watafute namna iliyo wazi ya kumpata mwekezaji ambaye anaweza kuendeleza zao la chai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako