• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuajiri walimu waliostaafu kufundisha katika shule za vijijini

    (GMT+08:00) 2019-05-03 18:20:15

    China inapanga kuwaajiri walimu 4,000 waliostaafu kufundisha wanafunzi wa shule zilizoko vijijini kati ya mwaka 2019 na 2020, ili kuboresha elimu katika sehemu hizo.

    Kutokana na taarifa iliyotolewa na wizara ya elimu ya China, mradi huo wa "Umri wa kifedha" ni kwa watu wenye umri chini ya miaka 65 ambao walikuwa walimu na wakuu wa shule.

    Taarifa hiyo inasema walimu wanaojitolea kufuatia mradi huo watafanya kazi kwa mwaka usiopungua mmoja, na wale watakaopita tathmini watahamasishwa kuendelea na kazi hiyo.

    Licha ya kufundisha, walimu hao pia watatathmini kazi za walimu wa shule za vijijini, kuwapa mafunzo, na kusaidia kuboresha uendeshaji wa shule hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako