• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA yatakiwa kuanzisha kituo cha kushughulikia mifumo ya mawasiliano

    (GMT+08:00) 2019-05-03 19:11:59

    Umoja wa Mawakala wa Forodha nchini Tanzania (TAFFA), Kanda ya Kaskazini, umeishauri Mamlaka ya Mapato (TRA), kuanzisha dawati maalumu la kushughulikia changamoto zinazowapata zikiwamo za mifumo ya mawasiliano ili kuwapunguzia gharama za kwenda mara kwa mara jijini Dar es Salaam.

    Katibu wa umoja huo Kanda ya Kaskazini, David Koyya, amesema, kumekuwa na mkanganyiko wa namna ya kuwasiliana na taasisi za serikali, wanapokuwa katika majukumu ya kuwahudumia wateja wao ambao wanapenda mizigo yao ifike kwa wakati. Kwa upande wake, mkurugenzi wa Kampuni ya Arusha Freight and Transport Agency Ltd, Aloyce Kilasara, alisema shughuli za upokeaji na usafirishaji wa mizigo zinapaswa kufanywa kwa weledi na kwa wakati, ili kuwawezesha wateja wao kufikia malengo yao. Alisema wakati mwingine wateja wao wamekuwa wakiwalalamikia kuchelewesha mizigo yao, wakati tatizo linakuwa ni ucheleweshaji wa nyaraka mbalimbali unaosababishwa na mifumo ya mawasiliano ya kompyuta kutofanya kazi kwa ufanisi muda wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako