• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwanda kimoja Kenya chafanikiwa kutengeneza dawa ya ukimwi

    (GMT+08:00) 2019-05-03 19:12:20

    Kiwanda kimoja nchini Kenya kimefanikiwa kutengeneza dawa za kupunguza makali ya ukimwi (ARVs) kwa kuzingatia mwongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO), na juma hili kiimetengeneza vidonge milioni tatu.

    Mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho kwa jina Universal Corporation, Perviz Dhanani alisema kwamba tayari walipokea vyeti kutoka kwa WHO kuwaruhusu kutengeneza vidonge hivyo kuanzia Novemba 2018.

    Kiwanda cha Universal ambacho kiko katika eneo la Kikuyu ni cha kwanza kupata idhini ya kutengeneza vidonge vya kupunguza makali ya Ukimwi Kenya.

    Asilimia 51 ya hisa za kiwanda hicho zilinunuliwa na kampuni ya Bangalore ambayo inamilikiwa na Pharma Strides Shasun mnamo mwaka wa 2016.

    Kiwanda cha Universal hutengeneza aina 100 za dawa ambazo huuzwa Kenya, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Namibia, Ivory Coast na Sierra Leone.

    Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Dawa na Sumu nchini (PPB) Bw Fred Siyoi alisema viwango vya kuzaliswa kwa dawa hizi humu nchini vimeboreshwa kutokana na kuzingatiwa kwa viwango vya uzalishajiwa na kufuatiliwa na mamlaka ya PPB. Kenya inatumia takriban Sh38 bilioni kila mwaka kuthibiti Ukimwi. Kila mgonjwa anatumia takribani Sh1,800 kila mwezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako