• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bajeti ya kaunti ya Kiambu yawashangaza maseneta

    (GMT+08:00) 2019-05-03 19:13:01

    Gavana wa kaunti ya Kiambu Ferdinand Waititu amewaacha maseneta kwenye hali ya mshangao, ilipobainika kuwa kaunti yake mwaka uliopita ilitenga bajeti ya kufadhili miradi ya kitaifa na kimataifa.

    Walipokuwa wakidurusu nakala za ukaguzi wa matumizi ya pesa ya kaunti ya Kiambu mwaka wa 2017/18, wakati gavana huyo alipofika mbele yao, wanachama wa Kamati ya Bunge la Seneti kuhusu matumizi ya pesa za umma walishangaa kuona kuwa serikali ya Gavana Waititu ilitumia zaidi ya Sh1 bilioni kufadhili miradi ya ikulu na serikali kuu.

    Katika nakala za kuonyesha jinsi kaunti hiyo ilitumia bajeti yake mwaka jana, maseneta waligundua kuwa kaunti ilitumia Sh902 milioni kufadhili shughuli za ikulu, Sh180 milioni kuwalipa marupurupu Marais Wastaafu, Sh573 milioni kwa shughuli za ushauri kwa mashirika ya serikali, Sh58 milioni kwa huduma za kutafuta amani nchini Sudan Kusini na Sh804 milioni zikatengwa (Sh493 milioni zililipwa), kufadhili mfumo wa elimu bila malipo kwa shule za msingi. Matukio hayo yaliwalazimu maseneta kwa sauti moja kutaka ukaguzi mpya ufanyiwe matumizi ya serikali ya kaunti hiyo mwaka jana, baada ripoti ya afisi ya Mkaguzi Mkuu kudai kuwa matumizi ya pesa katika kaunti hiyo yalikuwa sawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako