• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gazeti la Renminribao latoa tahariri ya kuadhimisha miaka 100 tangu Harakati ya Mei Nne

    (GMT+08:00) 2019-05-03 19:32:41

    Huu ni mwaka wa 100 tangu kufanyika kwa harakati ya Mei Nne.

    Gazeti la Renminribao la China leo limetoa tahariri ya "kufanya moyo wa Harakati ya Mei Nne ung'ae katika zama mpya", na kuwataka vijana wa sasa wa China wafanye juhudi kwa kulingana na matumaini ya chama, taifa na wananchi.

    Tahariri hiyo imesema, harakati hiyo ni tukio muhimu lenye maana ya kufungua ukurasa mpya wa historia ya China, na moyo wa harakati hiyo ni mali yenye thamani kubwa ya taifa la China.

    Mwaka 1919, kutokana na udhaifu wa serikali ya Beiyang ya China ambayo ilishinda Vita vikuu vya kwanza vya Dunia, kwenye mkutano wa Amani wa Paris, nchi za magharibi ziliamua kutoa mamlaka ya koloni la Ujerumani mjini Qingdao, China kwa Japan, hatua iliyowakasirisha sana wachina. Tarehe 4, Mei mwaka huo, baadhi ya vijana walianzisha harakati ya kizalendo kote nchini China, na kuleta mawazo ya Umarx, ambayo inafahamika kama Harakati ya Mei Nne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako