• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CMG yazindua maabara ya teknolojia za 5G, 4K na AI

    (GMT+08:00) 2019-05-05 18:49:54

    Hafla ya uzinduzi wa Maabara ya matumizi ya teknolojia za 5G, 4K na AI ya Shirika la Utangazaji la China CMG na shughuli ya kuanza kurekodi filamu za documentary "Miaka 30 ya Eneo la kiuchumi la Pudong, Shanghai" zimefanyika leo mjini Shanghai, China.

    Mkuu wa CMG Bw Shen Haixiong amehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa shughuli hizo, akisema tangu shirika la CMG lizinduliwe mwaka jana, limekuwa likishikilia kufuata kanuni na kutafuta uvumbuzi, kuimarisha matumizi ya teknolojia mpya, kukuza maendeleo ya mafungamano, na kuufanya mpangilio wa kimkakati wa matumizi ya teknolojia za 5G, 4K na AI uwe nguvu mpya ya kuhimiza maendeleo ya CMG.

    Ameongeza kuwa shirika la CMG litarekodi filamu za documentary "Miaka 30 ya Eneo la kiuchumi la Pudong, Shanghai" kwa kutumia teknolojia ya 4K, ili kuonyesha mafanikio makubwa ya eneo la Pudong yaliyopatikana katika miaka 30, na kuwafahamisha watu wengi zaidi historia ya mageuzi na kufungua mlango ya China na mustakabali wake mzuri katika zama mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako