• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuanzisha na kukamilisha mfumo wa maendeleo ya pamoja ya miji na vijiji

    (GMT+08:00) 2019-05-06 18:38:50

    Mkurugenzi wa Idara ya mikakati na mipango ya maendeleo iliyo chini ya Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bw. Chen Yajun amesema, maendeleo ya pamoja ya miji na vijiji ni injini yenye nguvu ya China katika kupanua maeneo ya maendeleo. Hivi sasa China inapanga kuanzisha mfumo kamili wa maendeleo ya pamoja ya miji na vijiji hadi ifikapo mwaka 2022, ili kuhimiza uchumi na jamii kupata maendeleo endelevu.

    Hivi sasa maendeleo ya pamoja ya miji na vijiji yamepata mafanikio ya kihistoria. Watu zaidi ya milioni 9 walioishi vijijini wamebadilika kuwa wakazi wa mijini, na mageuzi ya mfumo wa ardhi vijijini pia yamepata maendeleo mapya. Mbali na hayo, utaratibu wa bima ya matunzo ya uzeeni, matibabu, na magonjwa makubwa kwa wakazi wa miji na vijiji umeanzishwa hatua kwa hatua.

    Bw. Chen Yajun akizungumzia kuanzishwa kwa utaratibu kamili kuhusu maendeleo ya pamoja ya miji na vijiji amesema, utaratibu huo utaanzishwa kwa hatua ya mwanzo mwaka 2022, utaboreshwa zaidi ifikapo mwaka 2035 na kukamilishwa itakapofikia katikati ya karne ya 21. Akisema:

    "Malengo ya jumla ni kusukuma mbele mikakati ya uendelezaji wa vijiji na utandawazi wa miji ya aina mpya, kupunguza pengo la maendeleo, na kiwango cha maisha cha wakazi kati ya miji na vijiji, kuhimiza mawasiliano huru ya watu na vitu kati ya miji na vijiji, kufanya mgawanyo wa usawa wa maliasili ya umma, na kuharakisha mchakato wa kuanzisha uhusiano wa aina mpya kati ya miji na vijiji ulio wa kusaidiana, kupata maendeleo ya pamoja, ili kuharakisha mchakato wa kutimiza mambo ya kilimo cha kisasa na vijiji."

    Naibu mkurugenzi wa Idara ya mikakati na mipango ya maendeleo kwenye Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bibi Zhou Nan amesisitiza kuwa, China itaongeza nguvu katika kukamilisha mfumo wa pamoja wa bima ya jamii kati ya miji na vijiji. Anasema:

    "Bima ya matibabu na matunzo ya uzeeni zinafuatiliwa zaidi na wakazi wote wa mijini na vijijini, ambalo pia ni tatizo kubwa lililopo kwenye mchakato wa maendeleo kwa hivi sasa. Katika siku za baadaye, China itaharakisha hatua ya kutimiza vigezo vya pamoja kwa aina mbalimbali za bima za jamii, kuonesha umuhimu mkubwa wa bima hizo katika kuhakikisha maisha ya watu, na kurekebisha mgawanyo wa mapato ya jamii."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako