• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yaelekeza macho Amerika kusaka wafadhili

    (GMT+08:00) 2019-05-06 18:56:26
    Masuala kuhusu ustawi wa kiuchumi, uwekezaji na vita dhidi ya ufisadi yanatazamiwa kupewa kipaumbele maafisa wakuu wa Serikali ya Kenya watakapokutana na wenzao wa Amerika jijini Washington.

    Waziri wa Mashauri ya Kigeni, Bi Monica Juma ataongoza ujumbe wa serikali katika ziara hiyo nchini Amerika kuanzia Jumanne hadi Jumatano.

    Wizara hiyo ilisema, miongoni mwa watakaoandamana na Bi Juma ni maafisa wa ngazi za juu serikalini.

    Masuala ambayo yanalengwa kujadiliwa wakati wa ziara hiyo itakayohusisha mikutano na maafisa wa serikali ya Amerika ni kuhusu ushirikiano wa biashara na kiuchumi, masuala ya ulinzi, demokrasia na uongozi na yale yanayohusu ukanda huu.

    Katika ukuzaji wa uchumi, biashara na uwekezaji, Kenya na Amerika zinalenga kustawisha ushirikiano ambao utakuza uchumi kwa kuleta nafasi zaidi za ajira na uwezo wa kiufundi.

    Kenya pia inatazamia kutafuta ushirikiano mkubwa zaidi utakaoboresha biashara zinazoendelezwa chini ya Sheria ya AGOA inayotoa nafasi za ustawi wa kibiashara Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako