• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waajiri sasa waelekezwa usalama mahali pa kazi

    (GMT+08:00) 2019-05-06 18:58:20

    Waajiri nchini Tanzania wametakiwa kuzingatia utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi pamoja na sheria zingine za kazi ili kuboresha mazingira ya kazi kama walivyokumbushwa katika kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani na Rais John Magufuli. Mwenda amesema kuna kila sababu kwa waajiri hao kuzingatia agizo hilo la Rais kwa kuwa msingi wa utekelezaji wake upo kisheria na kwamba kinyume cha hapo na ukiukaji wa makusudi wa sheria hiyo iliyoanzishwa kwa lengo la kulinda afya na usalama wa wafanyakazi wawapo kazini. Alisema waajiri hawan abudi kutekeleza matakwa mengine ya kisheria ikiwamo kutoa mikataba ya ajira na kuruhusu uwapo wa vyama vya wafanyakazi katika sehemu za kazi.

    Wakati wa kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani mkoani Mbeya, Rais Magufuli aliwataka waajiri na wamiliki wa sehemu za kazi kuzingatia utekelezaji wa sheria za afya na usalama kazini, hatua itakayosaidia kuboresha mazingira ya kazi kwa kuyafanya kuwa mahali salama zaidi kwa wafanyakazi.

    Kauli hiyo ya Rais ilikuwa inajibu hoja mbalimbali zilizotolewa katika hotuba ya Shirikisho Huru la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) iliyowasilishwa katika sherehe hizo na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Dk. Yahya Msigwa, ambaye pamoja na mambo mengine alibainisha uwapo wa baadhi ya waajiri ambao hawazingatii masharti ya OSHA inavyoagiza.

    Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda

    Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda, alitoa wito huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akikazia agizo la Rais Magufuli kwa waajiri kuhusu utekelezaji wa sheria ya OSHA ya mwaka 2003 alilolitoa wakati wa sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mkoani Mbeya.

    Sheria hiyo ya OSHA imelenga kuwalinda wafayakazi dhidi ya madhara mbalimbali yanayoweza kuwapata wakiwa kazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako