• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tullow kuanza kuchimba mafuta baada ya kupata idhini ya NEMA

    (GMT+08:00) 2019-05-06 18:58:41

    Kampuni ya mafuta, Tullow itaanza kuchimba mafuta kwa kiwango kidogo eneo la Lokichar Kusini kuanzia wiki hii.

    Kampuni hiyo itachukua hatua hiyo baada ya kupokea idhini ya Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA).

    Katibu Mkuu wa Mafuta Andrew Kamau Ijumaa alisema Tullow inatarajiwa kusafirisha takriban mapipa 2,000 ya mafuta kila siku.

    Kutokana na hilo, Kenya itakuwa katika mkondo wa mataifa yanayouza mafuta ulimwenguni.

    Mzigo wa kwanza wa mafuta utasafirishwa kuanzia Juni, kabla ya uchimbaji kamili wa mafuta nchini kuanzia 2022.

    Kufikia sasa, Bw Kamau alisema zaidi ya mapipa 80,000 ya mafuta yamesafirishwa kutoka Lokichar hadi Bandarini Mombasa na yanangoja kuuzwa.

    Mapipa 200,000 ya kwanza yatauzwa kwa kampuni ya kusafisha mafuta itakayotoa bei ya juu, alisema Bw Kamau.

    Hata hivyo, alisema kuwa bado ni mapema kutambulisha wanunuzi. Maafisa wa Tullow na serikali walianza kukutana Machi kutafuta wanunuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako