• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri atoa angalizo hosteli za watalii porini

    (GMT+08:00) 2019-05-06 18:59:15

    Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu, ameuagiza uongozi wa Pori la Swagaswaga mkoani Dodoma, kumsimamia Mkandarasi anayejenga Hosteli ya kulala watalii wapatao 77 kutokana na Mkandarasi huyo kuwa na rekodi isiyoridhisha ya kutokumaliza majengo ya serikali.

    Pia, Ameutaka Uongozi huo kuwa makini na vifaa vya ujenzi anavyovitumia Mkandarasi huyo katika ujenzi wa jengo hilo utakaogharimu zaidi ya kiasi cha Sh. milioni 250 baada ya kubainika kuwa baadhi ya tofali zinazotumika kuwa chini ya kiwango.

    Kanyasu alifika katika jengo hilo na kujionea tofali zilizoandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo zikiwa zimekatika vipande vipande.

    Hali hiyo imemfanya Kanyasu kuagiza tofali hizo zikapimwe kwenye mamlaka husika kama zinakidhi viwango kwenye ujenzi wa jengo hilo.

    Katika hatua nyingine, Kanyasu alitembelea jengo la ofisi za Pori hilo ambalo linaendelea kujengwa katika eneo la Kwa mtoro na kuutaka uongozi huo kusimamia kwa ukaribu majengo yote yanayoendelea kujengwa kwa ajili ya manufaa ya Pori hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako