• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wazee wa China wenye umri wa miaka zaidi ya 60 yafikia milioni 249

    (GMT+08:00) 2019-05-07 17:40:18

    Mkutano wa viongozi wa ofisi ya mambo ya wazee ya China uliofanyika hivi karibuni mjini Beijing, ulichambua hali ya kuzeeka kwa watu wa China na kupanga kazi ya mambo ya wazee kwa mwaka huu nchini China.

    China ni nchi yenye idadi kubwa ya wazee duniani, na idadi hiyo inaendelea kuongezeka. Idadi ya wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 60 imefikia milioni 249, ambayo inachukua asilimia 17.9 ya wananchi wote wa China.

    Washiriki wa mkutano huo wameweka mkakati wa kuwapatia wazee wa China huduma zaidi ya kiafya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha na kuboresha mfumo wa kuwapatia wazee mijini na vijijini mafunzo na matunzo ya afya, kuhimiza huduma ya afya nyumbani, na kujenga mfumo wa utoaji wa huduma za muda mrefu kwa wazee wasioweza kuishi peke yao, na kuunganisha huduma za matibabu na matunzo kwa wazee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako