• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Benki Kuu imeshukisha viwango vya mikopo

    (GMT+08:00) 2019-05-07 19:55:41

    Benki ya Taifa ya Rwanda imerekebisha kiwango cha msingi cha kukopa kutoka asilimia 5.5 hadi asilimia 5 katika hatua iliyopangwa kuongeza mikopo kwa sekta binafsi.

    Kiwango hicho ndicho kiwango cah juu ambacho benki za kibiashara huwekeza fedha zao katika benki kuu.

    Hatua hii, ilitangazwa na Gavana wa Benki Kuu, John Rwangombwa, jana, muda mfupi baada ya mkutano wa Kamati ya Fedha.

    Kiwango hicho kilirekebishwa mnamo Desemba 2017 kutoka asilimia 6, ili kuhamasisha taasisi za fedha za mitaa kupunguza viwango ambavyo vinatoa mikopo kwa umma.

    Kupungua kwa kiwango cha kukopa fedha itajenga hali ambayo mabenki zitatengeneza mapato mengi kwa kuwekeza na sekta binafsi ikilinganishwa na wanapokuwa wakiwekeza na benki kuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako