• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Kirui, Kiplagat kuongoza timu ya riadha ya Kenya mashindano ya riadha ya dunia

    (GMT+08:00) 2019-05-08 08:41:30

    Kenya imetaja kikosi cha wanariadha tisa wakiwemo mabingwa wa dunia wa mwaka 2017 Geoffrey Kirui na Edna Kiplagat, kuiwakilisha nchi hiyo katika mbio za kilomita 42 kwenye riadha ya dunia zitakazofanyika Septemba 28 hadi Oktoba 6 mwaka huu jijini Doha nchini Qatar.

    Shirikisho la riadha la Kenya (AK) pia limemjumuisha kikosini Amos Kipruto ambaye alimaliza nafasi ya pili katika mashindano ya riadha ya Berlin mwaka jana.

    Wanariadha wengine walioitwa kikosini kwa upande wa wanaume ni Ernest Ng'eno, Laban Kokir na Paul Lonyangata, huku upande wa akina dada watakaoambatana na Edna ni Visiline Jepkesho, Sally Chepyengo na Ruth Chepng'etich. Kikosi hicho kitaanza mazoezi mapema Julai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako