• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Nene apanga kustaafu baada ya msimu huu kukamilika

    (GMT+08:00) 2019-05-08 08:42:17

    Mcheza kikapu Maybyner Rodney Hilário anayetambulika zaidi kama Nene na timu ya mpira wa kikapu ya Houston Rockets inayoshiriki ligi kuu ya kikapu Marekani (NBA) hawataendelea kuwekeana saini ya mkataba kwa msimu ujao wa ligi hiyo kutokana na mchezaji huyo kufikiria kustaafu kutokana na umri kuwa umeenda.

    Nene alikuwa ni mchezaji wa kwanza wa Brazil kuweza kuwepo katika ligi hiyo kwa msimu mzima na zaidi ya hapo bila kiwango chake kushuka. Mwaka 2011 Nene alisaini dau nono la dola za Marekani milioni 67 kuchezea timu ya Denver kabla ya kuuzwa kwa timu ya Wizards.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako