• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Pep Guardiola ashinda tuzo yake ya 7 EPL

    (GMT+08:00) 2019-05-08 08:43:01

    Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ametangazwa kuwa kocha bora wa mwezi April wa ligi kuu ya Uingereza (EPL) wakati huu wakiwa mbioni kutetea taji lao la ligi hiyo msimu wa 2018/2019, Guardiola ameiongoza Man City kushinda michezo yote mitano ya EPL ndani ya mwezi April.

    Pep Guardiola amefanikiwa kushinda tuzo hiyo ya kocha bora wa mwezi April kwa mara ya pili msimu huu na kwa mara ya saba toka amejiunga na Man City 2016 kama kocha mkuu, ndani ya April amefanikiwa kushinda michezo miwili migumu dhidi ya Manchester United uwanja wa Old Trafford na Tottenham katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako