• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali yaendelea na kampeni ya uzalishaji wa ndani

    (GMT+08:00) 2019-05-08 20:52:45

    Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini Tanzania (SIDO), limesema mwitikio wa mikoa katika kutekelezaji Programu ya wilaya moja bidhaa moja (ODOP) utachochea uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mazao ya kilimo na mifugo hapa nchini.

    Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mpango huo Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Prof.Sylvester Mpanduji, alisema utekelezaji wake umeanza kwa mafanikio baadhi ya mikoa.

    Alisema kuwapo kwa ODOP kumeamsha hali kwa wananchi kujikita katika uzalishaji zaidi hali inayochochea ukuaji wa uchumi na kufanikisha azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025 kwa vitendo.

    Amesema tayari ODOP imeweza kutekelezwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Singida, Mbeya, Dodoma, Manyara na Morogoro katika kuzalisha bidhaa zinazotokana na mazao ya kilimo na mifugo kama vile alizeti, mahindi, Mpunga na mazao ya mboga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako