• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China aongea kwa simu na falme wa Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2019-05-08 20:54:11

    Rais Xi Jinping wa China ameongea kwa njia ya simu na falme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz Al Saud.

    Kwenye mazungumzo hayo rais Xi ameeleza kuwa China inapongeza na kuunga mkono Saudi Arabia kuwa nchi mwenyeji wa mkutano wa kundi la nchi 20 kwa mwaka 2020, na inapenda kuimarisha uratibu na ushirikiano na Saudi Arabia, kuhimiza kwa pamoja kundi la nchi 20 kuchangia zaidi katika kulinda utaratibu wa pande nyingi, kujenga uchumi wa dunia ulio wazi, na kukamilisha usimamizi wa mambo ya uchumi ya dunia nzima.

    Naye mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud ameeleza kuwa Saudi Arabia inapenda kuendelea kutoa mchango kwa ajili ya kukuza uhusiano wa ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi za kiarabu, dunia ya kiislamu na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako