• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi kuu Tanzania Bara- Wekundu wa Msimbazi wawachakaza Wagosi wa Kaya 8-1, wakamata usukani wa ligi

  (GMT+08:00) 2019-05-09 07:56:55

  Simba Sports Klabu wanajulikana zaidi kama Wekundu wa Msimbazi, jana wamefanya mauaji kwa Wagosi wa Kaya Coastal Union ya Tanga kwa kuwachakaza magoli 8-1.

  Ni Emmanuel Okwi toka Uganda na Meddie Kagere toka Rwanda wameweza kupiga hat trick kwa kufunga bao 3 kila mmoja, huku Hassan Dilunga na Clatous Chama wakifunga goli moja kila mmoja.

  Simba sasa inashikilia uongozi wa ligi hiyo kwa kufikisha alama 81 wakiwashusha watani wao wa jadi Yanga yenye alama 80. Wakati huo huo, Kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems na mshambuliaji wa klabu hiyo John Raphael Bocco wameendelea kutawala katika tuzo za mwezi April, ambapo Aussems amepata tuzo ya ocha bora wa mwezi huo, huku Bocco amekuwa mchezaji bora wa mwezi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako