• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA:  Almanusura rungu liwashukie wachezaji wa Gor Mahia

    (GMT+08:00) 2019-05-09 08:00:51
    Kocha wa klabu ya Gor Mahia ya Kenya Hassan Oktay ameuomba uongozi wa klabu hiyo kutowaadhibu wachezaji wawili wa klabu hiyo Francis Kahata na Philemon Otieno kutokana na picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha wamelala sakafuni katika uwanja wa ndege wa Doha, Qatar walipokuwa safarini kuelekea Morocco kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho Afrika.

    Mara baada ya kurejea, mwenyekiti wa klabu hiyo Ambrose Rachier aliitisha kikao na waandishi wa habari na kueleza kuwa, wachezaji hao walifanya makusudi kuweka picha mitandaoni ili kuchochea hisia za huruma na kutoa taswira kuwa wanateseka. Hata hivyo, Oktay amewatetea wachezaji hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako