• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Klabu za Ulaya zapinga mageuzi ya Ligi ya Mabingwa

    (GMT+08:00) 2019-05-09 08:01:28
    Klabu za soka za Ulaya zimekitaka chama cha soka barani Ulaya (UEFA) kizishirikishe vizuri kwenye mipango yao ya kubadili mfumo wa ligi ya mabingwa ambao unaweza kuhakikisha timu vigogo zinacheza kwenye mashindano hayo mara kwa mara.

    Rais wa ligi kuu ya Uhispania Javier Tebas amesema iwapo UEFA itang'ang'ania kuendelea na mageuzi hayo yasiyohitajika, ana uhakika kesi yoyote itakayofunguliwa mahakamani itafanikiwa.

    Mabadiliko kwenye michuano ya klabu ya Ulaya yamegubikwa na utata baada ya rais wa chama cha vilabu vya Ulaya (ECA) Andrea Angelli kuwasilisha mapendekezo ya mfumo wa ligi moja ya Ulaya ambao kwa kiasi kikubwa utapunguza idadi ya timu zinazofuzu kutoka ligi za nchi wanachama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako