• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirikisho ya sekta mbalimbali ya Marekani yaipinga kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China zinazouzwa Marekani

    (GMT+08:00) 2019-05-09 17:59:07

    Serikali ya Marekani hivi karibuni imetangaza kwa dharura kuongeza ushuru wa forodha dhidi ya bidhaa za China zinazouzwa nchini Marekani kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kuanzia Mei 10. Uamuzi huo umepingwa na mashirikisho vya sekta mbalimbali ambayo pia yanaitaka serikali ya Marekani kuharakisha mchakato wa mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara na China, ili kufikia makubaliano mapema.

    Naibu mkurugenzi wa Shirikisho la wafanyabiashara wa mauzo ya rejareja la Marekani Bw. David French, amesema hatua ya kuongeza ushuru wa forodha itaathiri vibaya kampuni za Marekani haswa ndogo, na kusababisha upungufu wa nafasi za ajira nchini Marekani, na wateja wa Marekani pia wataathiriwa na mfumuko wa bei.

    Mkurugenzi wa Shirikisho la viwanda vya teknolojia ya habari Bibi Naomi Wilson, ameihimiza serikali ya Marekani kuendelea na mazungumzo na China na kufikia makubaliano ili kutoa fursa zaidi kwa kampuni hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako